PIKIPIKI nyingi zinazotoa huduma za usafiri wa abiria katika
mji wa Morogoro zimenyofolewa vioo ya upande 'Side Millor’ zinazowezesha dereva
kuona kitu kinachokuja nyuma yake akiwa barabarani hali inayohatarisha maisha ya dereva na abiria wa bodaboda.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia bodaboda nyingi ambaz ziko katika vituo mbalimbali vya bodaboda , umebaini kuwa kati ya pikipiki 10 zinazoengeshwa , saba hazina upande kioo, hali imezifanya kuwepo kwa idadi kubwa ya pikipiki zenye mapungufu hayo.
Mmoja wa madereva wa bodaboda, wa mtaa wa Mafisa Jumanne Mayala alisema yeye ameondoa upande kioo kwenye pikipiki yake ili kutokana na adha aliyokuwa anaipata anapotaka kupita maeneo yenye barabara nyembamba na kupenya kati kati ya magari.
“ Upande Kioo ama tunavyoita vioo vya pembeni , zinazuia uwezo wa
kupenya mwenye msongamano wa magari kutokana na upana wake “ alisema
Mayala.
Mbali na huyo, Dereva mwingine wa bodaboda wa mtaa wa Uguu , Kata
ya Uwanja wa Taifa aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Juma , alisema
yenye aliondoa ili kupata urahisi wa kuingiza pikipiki ndani ya chumba la kulaza kutokana na baadhi ya milango upana wake kuwa mdogo.
Juma alisema madereva wengi wa pikipiki za biashara maengesho yao ni
kwenye makazi wanakoishi.
Naye Dereva wa bodaboda mkazi wa Mwembesongo aliyejitambulisha kwa
jina la Charles Frank , alisema upande kioo katika pikipiki vina
umuhimu wake katika kusaidia usalama wa dereva na abiria .
Hivyo alisema kuondoa Upande Kioo mwa pikipiki ni makosa ya sheria
ya usalama barabarani na pia ni jambo hatarishi kwa mwendeshaji
kutokuwa salama akiwa barabarani.
“ Mara nyingi upande kioo vinasaidika kuona nyuma kitugani kinakuja
na kipo umbali gani na pia kusadia wakati wa kutaka kuingia upande
mwingine wa barabara bila kugeuka nyuma “ alisema Frank .
Kwa upande wake, Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa
Morogoro, Boniface Mbao , alisema kuwa, kuondoa upande kioo ‘ Side
Millor ‘ katika pikipiki ni kosa kisheria na kwamba opereshani
maalumu inaendelea kufanyika kuhusiana makosa hayo .
Mbao alisema , pikipiki za aina hiyo zinapokamatwa zinahesabika
zinaendeshwa barabarani zikiwa na ubovu na wakosaji wa makosa hayo
watatozwa adhabu kwa mujibu wa sheria za makosa ya usalama barabarani.

Kutokana na pikipiki kutozingatia
sheria za usalama barabarani, mwezi Mei katika operesheni iliyofanywa na polisi
wamekamata waendesha pikipiki 1,189 kwa kutoava kofia ngumu, 248 wanaendesha
bila bima, 168 hawana leseni na makosa mngine 955.
Mwisho.